Breaking News

:

HIZI NDO HATUA NNE ZA JINSI YA KUIANDAA JUISI YA UBUYU



JUISI YA UBUYU 
Juisi ya ubuyu ni moja kati ya juisi zilizopata wanywaji wengi duniani kote katika miaka ya hivi karibuni, Juisi ya ubuyu ina virutubisho vya calcium na Iron ambavyo ni muhimu katika miili yetu hasa kwa watoto,
wajawazito na wazee.
JINSI YA KUANDAA JUISI YA UBUYU

  1. Katika kuandaa juisi ya ubuyu unahitajika kuwa na ubuyu wa unga au wa mbegu, maji safi, sufuria, kijiko au mwiko, sukari, chujio, jagi na jiko.
  2. Kwa ubuyu wa unga;changanya vikombe 6 na maji vikombe 9.
  3. Kwa ubuyu wa mbegu; changanya vikombe 3 na maji vikombe 12.
  4. Weka sukari kiasi unachotaka, changanya vizuri na mwiko kisha bandika jikoni acha ichemke kwa kiasi cha kutosha ili kuuwa vijidudu vya magonjwa kama vitakuwemo na itakuwa tayari kwa matumizi.