MAHAKAMA YA RUFAA YAWARUDISHA JELA BABU SEYA NA PAPI KOCHA .
Wale wasanii maarufu wa rhumba wenye asili ya Kikongo nchini Tanzania, Nguza Viking a.k.a babu seya na mwanae Johnson Nguza a.k.a Papii kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto 10 wenye umri kati ya miaka 8 mpaka 10 waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Mashujaa iliyoko Sinza. Wataendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela. Hii ni kutokana na rufaa yao iliyokuwa ikisikilizwa mahakama ya rufaa leo kushindwa.