Breaking News

:

SAD NEWS! JULIUS NYAISANGA A.K.A ANKO J AMEFARIKI DUNIA.


Meneja wa Aboud Media, Julius Nyaisangah,ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio One, amefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Mazimbu Mkoani Morogoro.Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Nyaisanga alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na kisukari.
Wakati wa uhai wake, marehemu Nyaisanga aliwahi kufanya kazi sehemu mbali mbali ikiwemo katika makampuni ya IPP ambako alikuwa mkurugenzi wa Radio One pamoja na Radio Tanzania wakati huo ikiitwa RTD ambako alikuwa mtangazaji wa vipindi mbali mbali. Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.Mungu amlaze mahali pema peponi.