Breaking News

:

MASUALA MAKUU ATAKAYO HUTUBIA RAIS KIKWETE LEO JIONI BUNGENI.

Leo ni siku ambayo tunamsubiri  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuutubia taifa kupitia Bunge mjini Dodoma saa 10:00 jioni, itakuwa ni mara ya tano kuutubia bunge toka achaguliwa kushika madaraka. Mambo makuu ambayo Rais Kikwete anatarajiwa kuongelea leo ni pamoja
na masuala ya mchakato wa mabadiliko ya katiba, mgogoro unaofukuta ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pia huenda akazungumzia ni Operesheni Tokomeza Majangili na operesheni kimbuga, vile vile Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ni moja ya mambo ambayo Rais Kikwete atazungumzia leo hii mjengoni Dodoma.