MWILI WA MAREHEMU DKT SENGONDO MVUNGI KUWASILI NCHINI IJUMAA.
Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam. |
Mwili wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi unatarajiwa kuwasili nchini ijumaa, novemba 15, 2013, hii ni kwa mujibu wa tume ya Mabadiliko ya Katiba. Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini, baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha, siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013.
Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013. Mungu ailaze roho ya marehemu Dkt. Mvungi mahali pepeni, Amini.
Rais wa jamuhuri ya muungano dkt Jakaya Kikwete akimpa pole mke wa marehemu dkt Mvungi |