Breaking News

:

HUYU NDO MAREHEMU TABU LEY ROCHEREAU NA WIMBO WAKE WA MUZINA. MKONGO ALIYETUNGA NYIMBO 2000.

Tabu Ley Rochereau
Huu ni moja ya wimbo wa Tabu Ley Rochereau unaokwenda kwa jina la muzina, huu wimbo unanikumbusha enzi za utoto wangu, siku za sikukuu nilipokuwa ndani ya Mwanza, Mwanza club kwenye disco toto enzi hizo, hebu usikilize hapa chini tukiwa tunamuenzi mzee wetu aliyetutoka leo tarehe 30 mwezi wa 11 saa 8 am huko Belgium alipokuwa akitibiwa stroke aliyoipata mwaka 2008, Ikumbukwe ya kuwa Tabu ley amefariki akiwa na umri
wa miaka 72 na ni mwanamuziki aliye leta heshima katika muziki wa kiafrica toka aanze fani hii miaka ya 59 akiwa kama dansa, mtunzi na mwimbaji, akifanya kazi na kina Joseph Kabasele, Alias Grand Kalle na wengine wengi. Mpaka anakufa Tabu ley ametengeneza nyimbo zikadiliwazo 2000 zikiwa kwenye albam 250.