Breaking News

:

TANZANIA IKO TAYARI KUTUMIA SARAFU YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ?

 
JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI
Wakuu wa nchi zinazounda jumuiya ya Africa Mashariki watakutana leo tarehe 30 Novemba huko Kampala, Uganda. Wakuu hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya. Masuala watakayozungumzia leo ni
pamoja na soko la pamoja, umoja wa forodha, shirikisho la kisiasa na umoja wa sarafu ambapo leo watatia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja. Lengo la kuwa na sarafu moja ni kusaidia kupunguza gharama za shughuli za fedha ya utumiaji wa sarafu tofauti katika nchi zote tano na pia muungano wa fedha ni moja ya jitihada za kuunganisha nchi, vitu vyote tunavyovitafuta katika shirikisho vitafanikiwa kupitia muungano wa fedha. Swali la kujiuliza mpaka sasa ni kwamba Tanzania tuko tayari kuwa na sarafu moja ingawa ni mchakato wa utekelezaji utakaondumu ndani ya miaka kumi.