Breaking News

:

MWANAMKE HUPOTEZA MASAA 627 NA SEKUNDE 28 KWA MWAKA KUJIPAMBA TU.

 
masaa 627 na sekunde 28
Hii ni habari ya kushangaza lakini ukichunguza kwa makini utaona ina ukweli, hii ni kuhusiana na utafiti uliofanywa kwa wanawake 2000 na gazeti la daily mail, unao onyesha kuwa kwa mwaka mwanamke au
mwanadada hutumia masaa 627 na sekunde 28 kwa kujipamba tu na kujiweka katika mwonekano mzuri, hii ikiwa pamoja na kutafuta nini cha kuvaa , kuhofia mwonekano wake awapo mbele za watu,  kukabiliana na ongezeko la uzito wa mwili ili kumaintain mwili wake.

Kwa haraka ukifanya mahesabu ndani ya wiki moja hukaa kwa saa moja na dakika 46 kukabiliana na ongezeko la uzito wa mwili wake, dakika 50 kutafuta nguo za kuvaa, saa moja na dakika 32 kucheki alichochagua kimemtoa safi, dakika 32 kutafuta underwear za kuvaa na mengine mengi. Mwisho wa yote utangundua kuwa hutumia zaidi ya mwezi mmoja ndani ya mwaka katka kurekebisha mwonekano wake.