RAIS KABILA AFANYA ZIARA YA KWANZA ENEO LILILOKUWA LIKISHIKIRIWA NA WAASI WA M23.
![]() |
RAIS KABILA |
Rais wa jamhuri ya demokrasia ya Kongo, Rais Joseph Kabila amefanya ziara kwa mara ya kwanza maeneo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo yalikuwa yanashikiliwa na waasi wa M23 hadi
mapema mwezi huu. Akitumia muda wa wiki nzima kusafiri kilometer 930 (575 mile) huku akihutubia wakazi wa maeneo hayo mpaka kufika ngome ya kivu kasikazini iliyokuwa ikimilikiwa na M23, ambalo lina utajiri mkubwa wa madini. Katika ziara hiyo Rais Kabila aliongozana na waziri wa miundombinu na kudai kuwa ujenzi wa miundo mbinu iliyoalibiwa kwa vita iliyokuwa ikiendelea kwa miongo miwili na hii inaleta matumaini kwa nchi hiyo.