Breaking News

:

RAIS KENYATTA AZUNGUMZIA KUHUSU KUITENGA TANZANIA.


RAIS KENYATTA
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kulihutubia Bunge mjini Dodoma  Novemba 7, mwaka huu, kuhusu kutengwa kwa Tanzania na ushirikiano wa nchi tatu
zinazoundwa na Kenya, Uganda na Rwanda unaojulikana kama Umoja wa Walio Tayari, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema mradi wa ujenzi wa reli  wa kuanzia Mombasa, Kampala hadi Kigali, Rwanda utaijumuisha Tanzania kwa  kupitia Voi hadi Taveta kabla ya kuingia Tanzania ikianzia Moshi hadi Arusha.. Hayo aliyasema alipokuwa akizindua mradi huo pia Rais Kenyatta aliongeza kuwa katika miradi ya ujenzi wa barabara, Tanzania itahusishwa kwa kupitia Taveta na marekebisho ya barabara ya Lungalunga ya kupitia mpaka wa Horohoro nayo pia Tanzania itajumuishwa.