Breaking News

:

RAIS KIKWETE AONGEZA SIKU 14 KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.

 
JAKAYA MRISHO KIKWETE
Baada ya kifo cha mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya katiba, Dk Sengondo Mvungi kilichotokea Novemba 12, mwaka huu nchini Afrika Kusini, Tume ya mabadiliko ya katiba imeongezewa muda wa siku14 na Rais
Jakaya Kikwete ili kuiwezesha tume hiyo kumaliza kazi zake vizuri, ikumbukwe ya kuwa baada ya kifo cha Dkt Mvungi, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alitangaza kusitishwa kwa muda shughuli za Tume hiyo. Kwa sasa Tume itamaliza kazi yake, Desemba 30, mwaka huu badala ya Desemba 16 ambapo tume hiyo ilipaswa kumaliza kazi yake.