HII SIO VITA YA ZITTO KABWE NA CHADEMA ILA NI VITA YA ZITTO NA WATU WENGI.
![]() |
Zitto Kabwe |
Hayo si maneno yangu bali ni maneno ya mbunge wa Kigoma Kasikazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe alipohojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, akasema magenge yanayotaka urais mwaka
2015 na walioficha mabilioni ya fedha nje ya nchi ndio walioungana kutaka kumwondoa bungeni na kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao. Tuhuma 11 alizopewa na uongozi wa Chadema kwenye kikao cha waandishi wa habari zikimlenga yeye kusaliti chama hazifahamu na bado hajapewa na chama mpaka sasa.

Zitto aliendelea kufunguka kuwa kwenye kamati kuu alilaumiwa kwa masuala makuu matatu. La kwanza Ni kutokufanya kazi za chama, la pili kuwa nimemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akague vyama kutokana na kuwa na nia mbaya na chadema. la tatu ni kuhusu kukataa kupokea posho bungeni ambapo anadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzake wa chama hicho.