Breaking News

:

HOJA KUU TANO ZA KUMNG'OA SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA

Spika Anne Makinda
Hii ni hoja inayopangwa kurudishwa bungeni katika hili bunge lililoanza leo mjini dodoma na Mbunge wa Nzega Dkt Khamis Kigwangalla (CCM), Dkt Kigwangalla alisema anajipanga upya kuhahakikisha hoja ya
kumng’oa madarakani Spika wa Bunge, Anne Makinda inarejea tena bungeni licha ya kutupwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Katika hoja yangu nilichambua ukiukwaji uliofanywa na Spika Makinda kwa kutumia kanuni na sheria zilizopo, nilitarajia hoja ingeletwa bungeni lakini wameikataa.
Baadhi ya hoja alizozitoa katika Bunge lililopita ni pamoja na
  1. Spika amekuwa akikiuka kanuni za Bunge kwa kuzuia mijadala ya dharura na kutokutoa nafasi kwa hoja za wabunge kama kanuni zinavyoelekeza,
  2. kuzuia kwa mabavu majedwali ya mabadiliko ya sheria kwenye kamati ya bajeti,
  3. kuvunja masharti ya kanuni ya 48 inayotoa maelekezo ya namna ya kuwasilisha na kujadili jambo la dharura na kutumia madaraka vibaya,
  4. kumteua Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na kanuni zinazotaja wenyeviti kuchaguliwa na wajumbe wa kamati.
  5. Na kamati hiyo kulipwa posho ya Sh430,000 wakati kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
    Dkt Khamis Kigwangalla