KUTOKANA NA UMASIKINI RAPPER WALE ALISHINDWA KWENDA KWAO NIGERIA TOKA AZALIWE.
![]() |
Wale akiwa Nigeria |
Wale ni msanii wa hiphop mwenye asili ya Nigeria ambaye amezaliwa na anaishi Marekani, Olubowale Victor Akintimehin a.k.a Wale alizaliwa september 21, mwaka 1984 huko Washington DC, Marekani. Huku wazazi wake wote wawili wakiwa ni Raia kutoka Nigeria. Rapper huyu toka azaliwe hakuwahi kufika kwao Nigeria mpaka wiki iliyopita ndio kwa mara ya kwanza amekanyaga ardhi ya Nigeria.
Akizungumzia kuhusu hili suala Wale alisema alishindwa kutembelea kwao Nigeria kabla hajawa star kutokana na wazazi wake kushindwa kumudu gharama ya tiketi ya ndege ya kutoka Marekani kwenda Nigeria, waliishi kwa pato la $20,000 kwa mwaka ambapo ilimwiwia vigumu sana familia yake kuweka pesa ya tiketi ya ndege. Hata maisha waliyoishi na wazazi wake mitaa ya washington DC yalikuwa ya kimasikini, na alipofikisha miaka 15 alianza fanya vibarua ili kupata mahitaji yake madogo mpaka pale alipopata record deal na kuweza kumake mkwanja uliomfikisha hapo alipo.
![]() |
Don Jazzy, D'Banj, Wale, Olamide, na Kay switch |
Kwa hiyo vijana wenzangu msikate tamaa siku moja mambo yatanyooka kama Wale tuongeze juhudi.