HUYU NDO ASHA ROSE MIGIRO ALIYETEURIWA NA RAIS KUWA MBUNGE WA BUNGE LA TANZANIA.
![]() |
Dkt. Asha-Rose Migiro |
Dkt. Asha-Rose Migiro jana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mbunge katika Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mpaka kuteuliwa Dkt. Asha-Rose Migiro
alikuwa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi. Huu ni uteuzi wa pili wa rais Kikwete kumteua mbunge, wa kwanza ulikuwa ni wa Mhe. James Mbatia na uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
alikuwa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi. Huu ni uteuzi wa pili wa rais Kikwete kumteua mbunge, wa kwanza ulikuwa ni wa Mhe. James Mbatia na uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro alizaliwa tarehe 9 julai 1956 huko Ruvuma, Tanzania, na kupata elimu ya msingi shule ya Mnazi Mmoja mwaka 1963, baadae akahamia shule ya msingi Korogwe. Elimu ya sekondari alisoma katika shule ya Weruweru, akamalizia form five and six shule ya sekondari ya Korogwe mwaka 1975. Baadae alijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua shahada yake ya kwanza na ya pili kabla ya kujiunga na Chuo kikuu cha Konstanz kilichopo Ujerumani ambapo alisoma masomo ya udaktari mwaka 1992, ndipo akarudi kufundisha Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Dkt. Asha-Rose Migiro aliwahi kushika unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo aliteuliwa na Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon tarehe 5 Januari 2007. Hadi kuteuliwa kushika cheo hicho alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kushika wizara hiyo ya mambo ya nje ambayo iliyoshikwa awali na rais Kikwete mwenyewe chini ya raisi Benjamin Mkapa.