JE UNAFAHAMU ATHARI ZA KUTOKUNYWA MAJI?
Mwili wa binadamu umeundwa kwa asilimia 60 au 70 ya maji. Mtu asipo kunywa maji ya kutosha , inaweza kuleta athari katika mwili wake na kuathiri afya yake. Siku ya Leo katika hii kona ya Education, tutaangalia athari mtu anazoweza pata endapo hata kunywa maji ya kutosha. Maji husaidia kutoa sumu katika mwili na
kuvipa viungo muhimu ndani ya mwili unyevunyevu ili viweze kufanya kazi vizuri na kwa kushirikiana.
kuvipa viungo muhimu ndani ya mwili unyevunyevu ili viweze kufanya kazi vizuri na kwa kushirikiana.
DALILI ZA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI
Kama mtu hatokunywa maji au hatokunywa maji ya kutosha , anaweza kabiliwa na tatizo la dehydrated na dalili za hili tatizo la upungufu wa maji mwilini ni pamoja na;
- Kukauka na kunata kwa midomo,
- Macho kuingia ndani na Kutozalisha machozi ya kutosha,
- Kupata mkojo kidogo au kutokupata kwa siku kadhaa hii itasababisha kutokutoa uchafu utokao mwili wakati wa kukojoa,
- Kuhisi uchovu bila sababu,
- Kubana kwa misuli ya mwili,
- Chakula kutosagika vizuri mwilini na kuzuia mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri.
- kupata shinikizo la damu.
- Uzito kuongezeka na megine mengi.
NINI CHA KUFANYA.
Inasemekana kwamba watu wengi duniani wanaishi na tatizo la upungufu wa maji mwilini, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa NaturoDoc.com . Ili kuweza kuepuka hili Tatizo inashauriwa kwamba;