TAARIFA YA KUTOKA HOSPITALI YA MILLPARK ALIYOKUWA AKITIBIWA MAREHEMU DKT MVUNGI.
Milpark hospital |
Msemaji wa Hospitali hiyo, Tebogo Nyembezi alisema Dk Mvungi alicheleweshewa tiba baada ya kupata
tatizo la maji hayo yanayotunza ubongo kumwagika mara baada ya kujeruhiwa.
tatizo la maji hayo yanayotunza ubongo kumwagika mara baada ya kujeruhiwa.
Dk Mvungi (61), alipata majeraha makubwa baada ya kujeruhiwa na watu waliovamia nyumbani kwake Kibamba, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Novemba 3 mwaka huu. Alifariki dunia jana mchana.
“Maji hayo ambayo ni miligramu 50 tu katika ubongo wa mwanadamu ambayo huufanya ubongo uelee yakimwagika nusu tu, basi mgonjwa yupo hatarini, lakini akiwahishwa na kupata tiba sahihi anaweza kupona,” alisema Nyembezi.
Alisema iwapo mgonjwa atapewa tiba sahihi ndani ya saa 48, ubongo wake unaweza kurudi katika hali ya kawaida, lakini saa hizo zikizidi hawezi kupona kabisa kwa sababu maji hayo yanapomwagika ubongo hujigonga kwenye mifupa ya sakafu yake na kuharibika kabisa.