Breaking News

:

PINDA AMWOMBEA ZITTO KABWE KUEPUSHWA NA BALAA LA KUSEMA UONGO.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda aliyasema hayo jana Bungeni katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu  “Nadhani Mwenyezi Mungu atamwepusha Zitto na balaa zinazoweza kumpata kwa
kusema uongo”, hii ni kutokana na Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini  kwa tiketi ya chama cha Chadema kusema katika mikutano mbalimbali ya hadhara kuwa Waziri Mkuu analipwa mshahara wa Sh milioni 26 kwa mwezi huku Rais akilipwa Sh milioni 32.

Mshahara anaopata Waziri Mkuu ni Sh milioni 6 na hiyo ni pamoja na posho ya mke wake, Pinda aliongeza kwa kusema  ukiongeza posho ya Sh 500,000 na Sh 600,000 ya uwajibikaji  kwa kuwa ni Waziri Mkuu. Maneno hayo Pinda aliyasema alipokuwa akitoa ufafanuzi alioombwa kuutoa na Spika wa Bunge, Anne Makinda  kutokana na Swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mkanyageni kwa tiketi ya chama cha CUF, Mhe. Habib Mnyaa kwa kutaka kupata ufafanuzi kuhusu Mshahara wa Rais na Waziri Mkuu unaoongelewa katika mitandao ya kijamii.