Breaking News

:

RAIS KIKWETE ATUONGOZA VIZURI KWENYE MAZISHI YA NELSON MANDELA.

MAZISHI YA NELSON MANDELA.
Leo ni siku ambayo Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela anazikwa kijijini kwao Qunu ambapo inakadiliwa watu wapatao 4500 wameuzulia katika mazishi haya huku wakiimba na kuomboleza. Maziko hayo ya  Mandela aliyefariki desemba 5 akiwa na umri wa miaka 95 yatakuwa ya kijadi huku Jeneza la
mandela likiingia likiwa limefunikwa bendera ya Afrika kusini katka gari la kubebea mizinga ya bunduki kutoka nyumbani kwake kuelekea mahali ambapo Mndela atazikwa.

Wajukuu wawili wa Mandela Ndaba na Nandi walisoma historia ya babu yao huku mjane wa Mandela  Graca Machel, na mke wake wa zamani, Winnie-Madikizela Mandela, wamekaa karibu na rais Jacob Zuma. Viongozi kutoka mataifa mbalimbali wametoa salamu zao, Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameelezea hitoria fupi ya Mandera alivyokuwa na uhusiano mzuri na Tanzania. Nae rais wa zamani wa Zambia, Kenneth David Kaunda mwenye umri wa miaka 89 ametoa salamu zake na kumaliziwa na rais wa Afrika kusini  Jacob Zuma.